SUMAJKT CONSTRUCTION COMPANY LIMITED (SUMAJKT CCL)
SUMAJKT CCL ni moja ya Kampuni Tanzu za Shirika la Uzalishaji Mal la Jeshi la Kujenga Taifa.
Kampuni hii inayojishughulisha na kazi za Ujenzi hapa nchini.
Kazi zinazotekelezwa na Kampuni ya Ujenzi ya SUMAJKT (SUMAJKT Construction Company Limited)
a. Ujenzi wa Nyumba za Makazi, maofisi na biashara.
b. Ujenzi wa barabara na madaraja.
c. Ujenzi wa Mabwawa ya maji na miundombinu ya maji.
d. Kazi zote za Umeme katika Majengo.
e. Kazi za Uhandisi wa Mitambo.
f. Kazi za Umeme mkubwa.
OFISI ZA KAMPUNI
5. Makao Makuu ya Kampuni yapo Dar es Salaam eneo la Mlalakuwa na ili kurahisisha utendaji nchini shughuli za ujenzi zimegawanywa katika Kanda saba (7) za ujenzi kama ifuatavyo:-
a. Kanda ya Mashariki (Eastern Zone)
Kanda hii inajishughulisha katika utekelezaji wa kazi za ujenzi kwa Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Pwani.
b. Kanda ya Kusini Nyanda za Juu
(Southern Western Zone)
Kanda hii inajishughulisha katika utekelezaji wa kazi za ujenzi kwa Mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Njombe na Songwe.
c. Kanda yaKaskazini (Northern Zone)
Kanda hiiinajishughulishakatikautekelezajiwa kazizaujenzikwaMikoayaArusha, Kilimanjaro,
Manyarana Tanga.
d. Kanda ya Ziwa (Lake Zone)
Kanda hii inajishughulisha katika utekelezaji wa
kazi za ujenzi kwa Mikoa ya Mwanza, Shinyanga,
Geita, Kagera, Mara na Simiyu.
e. Kanda ya Kati (Central Zone)
Kanda hii inajishughulisha katika utekelezaji wa
kazi za ujenzi kwa Mikoa ya Dodoma na Singida.
f. Kanda ya Kusini (Southern Zone)
Kanda hii inajishughulisha katika utekelezaji wa
kazi za ujenzi kwa Mikoa ya Mtwara, Lindi na
Rukwa.
g. Kanda ya Magaribi (Western Zone)
Kanda hii inajishughulisha katika utekelezaji wa
kazi za ujenzi kwa Mikoa ya Katavi, Tabora na
Kigoma.
Dira na Dhamira ya SUMAJKT CONSTRUCTION COMPANY LIMITED
Dira
Kuwa Kampuni ya Umma ya Ujenzi inayoaminiwa kwa ukuaji wa Miundombinu Tanzania.
Dhima
Kutoa Huduma na bidhaa za Ujenzi zinazokidhi viwango stahiki katika muda uliowekwa kwa kutumia Teknolojia muafaka.
TUNU
- Weledi
- Uadilifu
- Uwazi
- Uwajibikaji
- Kazi pamoja